Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 15:34

Rwanda yamuhukumu miaka 20 jela mzee wa miaka 75 kwa mashtaka ya mauaji ya kimbari


Venant Rutunga, mshtakiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda
Venant Rutunga, mshtakiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda

Rwanda imemkuta na hatia mzee mwenye umri wa miaka 75 kwa kushiriki katika mauaji ya kimbari ya 1994, na kumuhukumu miaka 20 jela, chombo cha habari kinachoungwa mkono na serikali kiliripoti Alhamisi.

Venant Rutunga alirejeshwa kutoka Uholanzi hadi Rwanda mwaka 2021, ambako alifikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kuelekeza mauaji katika robo karne iliyopita.

Mwendesha mashtaka alisema mashahidi walimhusisha Rutunga kwa kuwaleta maafisa wa polisi kwenye taasisi ya utafiti wa kilimo (ISAR), ambako aliwahi kuwa mkurugenzi wa mkoa, kupelekea wafanyakazi Watutsi na wale waliotafuta hifadhi huko kuuawa.

Kitengo cha Mahakama Kuu ya Uhalifu wa Kimataifa kilimuhukumu “Venant Rutunga” miaka 20 jela kwa kuhusika kwake katika mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi,” kulingana na chombo cha habari kinachoungwa mkono na serikali, New Times.

“Mahakama ilimkuta Rutunga na hatia ya kuwa mshiriki wa mauaji ya kimbari, “New Times iliripoti.

Awali, mshtakiwa huyo alikabiliwa na mashtaka matatu: mauaji ya kimbari, kushiriki katika mauaji ya kimbari, na kushiriki katika mauaji ya kuangamiza kama uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Hata hivyo, jopo la majaji watatu liliamua kwamba hakuna ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa Rutunga alishiriki binafasi katika mauaji au kutoa silaha.

Waendesha mashtaka walikuwa wameomba kifungo cha maisha.

Rutunga ambaye alikana mashtaka dhidi yake, alidai kuwa aliwaita maafisa hao wa polisi ili kulinda usalama wa taasisi hiyo, uamuzi ambao amesema uliidhinishwa na bodi ya wakurugenzi ya ISAR.

Forum

XS
SM
MD
LG