Raia wameambiwa kuwa sababu ya ushauri huo ni kutokana na kukabiliwa na hatari ya kuandamwa na mamlaka za Marekani.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia Maria Zakharova, amesema uhusiano wa Russia na Marekani uko katika hali ya kuvunjika kabisa.
Wanadiplomasia wa Russia na Marekani wanasema uhusiano kati ya nchi hizo mbili ni mbaya sana kuliko ilivyowahi kuwa tangu kutokea mgogoro wa makombora ya Cuba mwaka 1962.
Uhusiano umeharibika kutokana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine, na ulifikia kiwango kibaya zaidi mwezi uliopita baada ya Ukraine kuanza kutumia makombora ya masafa marefu ya Marekani na Uingereza.
Hatua ya Ukraine kutekeleza mashambulizi ndani ya Russia imepelekea Russia kufanyia marekebisho sheria zake za matumizi ya silaha za nyuklia.
Forum