Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 15:58

Russia yasema mfanyakazi wa zamani wa ubalozi mdogo wa Marekani ameshtakiwa kwa ujasusi


Picha hii iliyotolewa kutoka katika video iliyochukuliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Lefortovo, inamuonyesha Robert Shonov akifikishwa mahakamani.
Picha hii iliyotolewa kutoka katika video iliyochukuliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Lefortovo, inamuonyesha Robert Shonov akifikishwa mahakamani.

Shirika la Usalama la Russia FSB lilisema Jumatatu mfanyakazi wa zamani wa ubalozi mdogo wa Marekani huko Vladivostok amefunguliwa mashtaka yanayohusiana na shutuma kuwa  alikusanya taarifa kuhusu vita nchini Ukraine na maadamano mbalimbali nchini Russia kwa niaba ya Marekani.

Taarifa ya FSB ilisema Robert Shonov alikusanya taarifa kuanzia Septemba 2022, ikiwemo kampeni ya Russia kusajili wanajeshi.

Mnamo mwezi Mei, Wizara ya Ulinzi ya Marekani ililaani taarifa ya kukamatwa kwa Shonov, ikisema kuwa madai hayo dhidi yake “hayana ukweli wowote.”

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Mathew Miller alisema katika taarifa yake kuwa Shonov alifanya kazi katika ubalozi mdogo kwa zaidi ya miaka 25 kabla ya kuajiriwa na shirika la nje ambalo linatoa huduma kwa ubalozi wa Marekani mjini Moscow.

“Jukumu la Bw. Shonov hadi wakati anakamatwa lilikuwa kukusanya habari za vyombo vya habari zilizoko katika vyanzo mbalimbali vya habari vya Russia,” Miller alisema.

“Mtu huyu analengwa chini ya sheria ya “ushirikiano wa siri” unaoonyesha jinsi serikali kuu ya Russia inavyoongeza utumiaji wa sheria kadamizi dhidi ya raia wake.”

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii zinatokana na mashirika ya habari ya Associated Press, Agence France-Presse na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG