Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 07:38

Russia yaishambulia mikoa kadhaa ya Ukraine kwa droni 35


Athari za droni za Russia zilizo shambulia mkoa wa Kyiv.
Athari za droni za Russia zilizo shambulia mkoa wa Kyiv.

Jeshi la Ukraine lilisema Alhamisi majeshi ya Russia yameshambulia mikoa kadhaa usiku kucha yakitumia ndege zisizo kuwa na rubani 35.

Jeshi la anga la Ukraine lilisema kuwa mfumo wa ulinzi wa anga ulitungua droni zote isipokuwa moja tu, huku hayo yakifanyika katika anga ya Kyiv, Dnipropetrovsk, Kherson, Mykolaiv, Chernihiv na maeneo mengine.

Hakuna ripoti za vifo au uharibifu katika maeneo mashambulizi yalipotokea.

Katika mji wa kusini wa Nikopol. Katika mkoa wa Dnipropetrovsk, maafisa walisema kombora la Russia limeua watu wawili.

Gavana wa mkoa Serhiy Lysak alisema kwenye mitandao ya kijamii kuwa mwanaume mwenye umri wa miaka 86 pia alipelekwa hospitali.

Lysak alisema shambulizi lililofanywa na Russia limeharibu nyumba za makazi kadhaa na majengo ya shambani.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii imetokana na AFP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG