Rais wa Russia, Vladimir Putin, anaonekana kuwa na matumaini ya msukumo wa kijeshi na kubadilika kwa hali ya masuala kwa mataifa ya magharibi na kujikita zaidi kwenye vita vya Israel na Hamas vitampa fursa kwa harakati zake za Ukraine, zinazo karibia mwaka wa pili sasa.
Baada ya kuwepo ishara ya kudorora kwa msaada wa mataifa ya magharibi kwa Ukraine, Russia imeongeza nguvu yake dhidi ya vikosi vya Ukraine katika maeneo kadhaa ya mapambano ya zaidi ya kilometa 1,000.
Shauri la kuipatia Ukraine, misaada zaidi linasuasua katika bunge la Marekani, wakati wa Republikan, wanasisitiza kuhusishwa pia na fedha zaidi ili kuongeza nguvu katika mpaka wake na Mexico, jambo linalopingwa na Wademokrat.
Forum