Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:45

RSF yatajwa kuwa kundi la waasi Sudan


Moshi mkubwa ukifuka juu ya majengo yaliyoko jirani na uwanja wa ndege wa Khartoum mnamo tarehe 15, Aprili 2023, Picha na AFP.
Moshi mkubwa ukifuka juu ya majengo yaliyoko jirani na uwanja wa ndege wa Khartoum mnamo tarehe 15, Aprili 2023, Picha na AFP.

Mkuu wa jeshi la Sudan Jumatatu alikitaja kikosi cha kijeshi cha Rapid Support Forces kuwa ni kikundi cha waasi na kuamuru kivunjwe.

Wakati sehemu ya kundi hilo likipambana na jeshi katika ghasia mbaya zilizosababisha kuondoka kwa utawala wa kiraia na kuifanya Marekani kutoa wito wa kusitisha mapigano.

Pande zote mbili zilidai zilipata mafanikio siku ya Jumatatu, katika vurugu za kugombea madaraka zilizosambaa nchi nzima Kundi la wanaharakati la Kamati Kuu ya Madaktari wa Sudan limesema kuwa takriban raia 97 na askari 45 wameuwawa na jumla ya watu 942 wamejeruhiwa, tangu mapigano yalipoanza mwishoni mwa wiki.

Serikali haijachapisha idadi kamili iliyotokana na mapigano hayo ambayo yamezua hofu ya kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Siku ya Jumatatu, ulipuaji mabomu na mashambilizi ya ndege za kivita yaliutikisa mji wa Khartoum, pamoja na eneo jirani la makao makuu ya jeshi, na katika eneo la Bahri ililipo ng'ambo ya mto Nile, jirani na kambi nyingine ya jeshi, walioshuhudia mashambilizi hayo walisema.

Moshi ulitanda kwenye njia za kuruka ndege kwenye uwanja wa ndege wakimataifa katika mji mkuu, ambako milipuko na moto ilionekana kwenye picha za televisheni.

Moshi ukionekana kwenye uwanja wa ndege wa Khartoum, tarehe 15 Aprili 2023. Picha na shirika la habari la AFP.
Moshi ukionekana kwenye uwanja wa ndege wa Khartoum, tarehe 15 Aprili 2023. Picha na shirika la habari la AFP.

Mapambano hayo ya nadra yalizuka katika mji mkuu na kusambaa katika maeneo mengine ya Sudan, na kusababisha mapambano kati ya jeshi dhidi ya kikosi cha Rapid Support Forces (RSF), kundi la wanamgambo ambalo lilitarajiwa kuungana na jeshi ambapo viongozi wake wanashiriana madaraka katika baraza utawala la kijeshi.

Mkuu wa jeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ambaye ni kiongozi wa baraza la utawala wakati kiongozi wa RSF Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana kama Hemedti, ni naibu wake. Pande zote mbili zilisema zimepata mafanikio siku ya Jumatatu.

Kundi la RSF lliidai kuuteka uwanja wa ndege na kambi ya jeshi, wakati jeshi lilisema linadhibiti makao yake makuu licha ya kile ilichokiita "mapigano madogo" katika maeneo jirani. Shirika la habari la Reuters lilithibitisha video inayoonyesha vikosi vya RSF vilivyokuwa katika baadhi ya maeneo hayo lakini haikuweza kuthibitisha madai ya habari katiak uwanja wa mapambano.

Jeshi limeweza kupata tena udhibiti wa kituo kikuu cha televisheni, ambacho kilizimika kwa muda mfupi baada ya milio ya risasi kusikika wakati wa urushaji wa matangazo mubashara. Kituo kilianza kurusha matangazo ya video zikilionyesha jeshi likiharibu magari ya RSF, siku moja baada ya RSF kusema ilikuwa imeliteka jengo hilo.

Chanzo cha bahari hii ni shirika la habari la Reuters.

XS
SM
MD
LG