Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 29, 2024 Local time: 09:09

Ramaphosa aapishwa tena kuwa rais wa Afrika Kusini


 Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akichukua kiapo cha kuwa rais wa nchi hiyo huko Pretoria Juni 19, 2024. Picha na Kim LUDBROOK / AFP)
Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akichukua kiapo cha kuwa rais wa nchi hiyo huko Pretoria Juni 19, 2024. Picha na Kim LUDBROOK / AFP)

Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa ametoa wito kwa nchi kusonga mbele kwa pamoja wakati akitoa hotuba yake alipokuwa akiapishwa kuongoza nchi kwa muhula wake wa pili huko Pretoria.

Ramaphosa ameapishwa Jumatano baada ya chama chake cha ANC kushindwa nguvu na kulazimika kufikia makubaliano ya kuunda serikali ya muungano mwishoni mwa wiki iliyopita.

Jaji mkuu Raymond Zondo aliongoza kiapo cha Ramaphosa mbele ya wabunge , viongozi kutoka mataifa mbalimbali, na viongozi wa kidini na kitamaduni huku wafuasi wake wakishangilia katika majengo ya serikali kuu, Union Buildings.

Wabunge walipiga kura kwa wingi kumchagua tena Ramaphosa mwenye umri wa miaka 71 wiki iliyopita baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Mei 29 ambao hakuna chama kimoja kilichopa ushindi mkubwa kuunda serikali pekee yake.

Takriban viongozi wa dunia 18 walihudhuria sherehe hizo wakiwemo marais wa Nigeria Bola Tinubu, Angola Joao Lourenco, Congo Brazavile Denis Sassou Nguesso na Eswatin mfalme Mswati III.

Katika hotuba yake Ramaphosa alisisitiza kwamba kuundwa kwa serikali ya muungano kuwa ni mwanzo mpya.

“wakati tunaingia katika enzi mpya ya taifa letu, ukakamavu wa demokrasia yetu imeptia mtihani mwengine na watu wameamua kwa sauti kwamba wanachagua amani na demokrasia dhidi ya migogoro, vurugu, mbinu zinazokwenda kinyume cha demokrasia na katiba,” alisema Ramaphosa.

Forum

XS
SM
MD
LG