Rais Cyril Ramaphosa anawania muhula wa pili kama kiongozi wa taifa hilo lililoendelea zaidi kiviwanda barani Afrika, lakini chama chake cha ANC kimekuwa dhaifu baada ya kushindwa kupata wingi wa viti bungeni kwenye uchaguzi wa Mei.
Hilo lina maana kwamba atahitaji uungaji mkono wa vyama vingine ili kushinda urais kwa mara nyingine. ANC kinatumai kuwa ushirikiano na vyama vingine na hasa kile cha Democratic Alliance, DA utampa ushindi tena. Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, ANC Alhamisi jioni kilitangaza kukubaliana na Democratic Alliance, pamoja na vyama vingine vidogo, wakati katibu wake Fikile Mbalula, akisema kuwa walikuwa karibu kukamilisha mazungumzo hayo.
DA ambacho kilishika nafasi ya pili kwenye uchaguzi huo kimesema kuwa mashauriano yaliendelea hadi saa za usiku kabla ya bunge kukutana leo saa 4 za asubuhi kwa saa za huko.
Forum