Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 22:37

Rais wa zamani wa Marekani akabiliwa na madai ya udanganyifu yanayotishia kuvunja himaya ya biashara yake


Michael Cohen, kushoto, na Donald Trump, kulia
Michael Cohen, kushoto, na Donald Trump, kulia

Michael Cohen, Wakili wa zamani wa Donald Trump na mpambe wake, anatarajiwa kufika mahakamani kutoa ushahidi  Jumanne kama shahidi mkuu dhidi ya rais wa zamani katika kesi ya madai ya udanganyifu ambayo inatishia kuvunja himaya ya biashara ya Trump.

Trump anatarajiwa kuwepo mahakamani Jumanne, kulingana na mtu anayefahamu mipango yake. Hilo linaweza kupelekea kuwepo hasira wakikutana uso kwa uso na Cohen, ambaye amekuwa ni mkosoaji mkubwa kabisa wa Trump tangu walipokata mawasiliano miaka mitano iliyopita.

Trump, mgombea anayeongoza katika kuwania uteuzi kugombea urais kwa chama chake cha Republikan, siku ya Jumatatu alikuwa katika kampeni huko New Hampshire na siku chache baada ya jaji anayesikiliza kesi yake kumpiga faini ya dola 5,000 kwa kukiuka amri ya kutokosoa wanaohusika katika kesi yake.

Kesi hiyo iliyowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa New York Mdemokratik Letitia James inadai Trump alipunguza thamani ya mali zake kwa mabilioni ya dola katika taarifa aliyowasilisha katika mabenki ili kupata mikopo wa masharti bora zaidi.

Cohen alikuwa wakili waTrump binafsi na anayetumia hila kwa miaka mingi kabla ya kukata uhusiano katikati ya matatizo ya kisheria yaliyokuwa yanamkabili.

Trump amekanusha kufanya kosa lolote na kutetea tathmini ya mali zake, akisema kesi hiyo ya “ulaghai” ni kumuandama kisiasa.

Katika baadhi ya nyakati amefika mahakamani katika kipindi cha mwezi uliopita, akilalamika kwa maneno makali kwa waandishi kuwa ni kizuizi katika kampeni yake.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG