Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 16:23

Wakili wa zamani wa Trump Michael Cohen atoa ushahidi mbele ya jopo la mahakama ya Manhattan


Michael Cohen, wakili wa zamani wa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, akiwasili katika Mahakama ya New York katika Jiji la New York, Marekani, Machi 13, 2023. REUTERS
Michael Cohen, wakili wa zamani wa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, akiwasili katika Mahakama ya New York katika Jiji la New York, Marekani, Machi 13, 2023. REUTERS

Wakili wa zamani wa Donald Trump Michael Cohen alitoa ushahidi wake Jumatatu mbele ya jopo la mahakama ya Manhattan, mjini New York, lililokuwa likichunguza malipo ya pesa yaliyofanywa kwa niaba ya rais huyo wa zamani.

Rafiki huyo wa karibu wa Trump aligeuka kuwa hasimu, alitumia karibu masaa matatu kujibu maswali katika kesi inayofanyika kwa faragha. Anatarajiwa kurejea tena kwa ushahidi zaidi kesho Jumatano, wakili wake alisema wakati wawili hao wakitoka katika mahakama.

Ushahidi huo unakuja wakati muhimu, huku ofisi ya wakili wa wilaya ya Manhattan ikitathmini iwapo itatafuta mashtaka dhidi ya Trump kuhusu malipo yaliyotolewa wakati wa kampeni yake ya 2016 kwa wanawake wawili ambao walidai kuwa na uhusiano wa kimapenzi au ngono naye. Nia mpya ya Stormy Daniels na malipo ya Dola 130,000 aliyopokea kabla ya uchaguzi wa urais wa 2016 inakuja wakati muhimu kwa Trump, ambaye anawania uteuzi wa urais wa chama cha Republican kwa mwaka wa 2024. Daniels amesema alipokea malipo hayo kwa kubadilishana na kutota taarifa yeyote juu ya masuala ya ngono na uhusiano na Trump, ambaye anakanusha lolote kutokea kati yao.

XS
SM
MD
LG