Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 12, 2025 Local time: 01:25

Rais wa Venezuela aiomba Mahakama ya Juu kufanya ukaguzi wa uchaguzi wa rais wenye utata


Rais wa Venezuela akizungumza nje ya Mahakama ya Juu, mjini Caracas, Julai 31, 2024
Rais wa Venezuela akizungumza nje ya Mahakama ya Juu, mjini Caracas, Julai 31, 2024

Rais wa Venezuela Nicholas Maduro amesema aliiomba Mahakama ya Juu ya nchi hiyo kufanya ukaguzi wa uchaguzi wa rais, baada ya viongozi wa upinzani kupinga madai yake ya ushindi na huku kukiwa wito wa jumuia ya kimataifa kutangaza hesabu za kina za kura.

Maduro aliwambia waandishi wa habari Jumatano kwamba chama tawala kiko pia tayari kuonyesha karatasi zote za kuhesabu kura za uchaguzi wa Jumapili.

“Nimejifikisha mwenyewe mbele ya mahakama,” aliwambia waandishi wa habari nje ya makao makuu ya Mahakama ya Juu mjini Caracas, na kuongeza kuwa “yuko tayari kuitwa, kuhojiwa, kuchunguzwa.”

Mpinzani mkuu wa Maduro, Edmundo Gonzalez, na kiongozi wa upinzani Maria Corina Machado, wanasema walipata zaidi ya theluthi mbili ya kura zilizohesabiwa ambazo kila machine ya kupigia kura kwa mfumo wa kielektroniki ilizishapisha baada ya zoezi la uchaguzi kumalizika.

Forum

XS
SM
MD
LG