Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:08

Magufuli 'amtumbua' waziri wa habari


Rais John Magufuli
Rais John Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemfukuza kazi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na kumweka Dkt Harrison George Mwakyembe katika nafasi hiyo kufuatia mabadiliko madogo alioyafanya katika Baraza la Mawaziri.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu Dar es Salaam, katika mabadiliko hayo Rais amemteua Prof Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Aidha Rais amemteua Dkt Harrison George Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Taarifa hiyo inasema uteuzi huo unaanza mara moja.

Wateule wote wataapishwa Ijumaa, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Nape Nnauye aliyekuwa anashikilia wadhifa kama waziri wa wizara ya habari ametumbuliwa baada ya kupokea ripoti Jumatano kuhusu uvamizi uliofanywa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika studio za kituo binafsi cha habari cha Clouds mwishoni mwa wiki.

Kamati iliyokuwa imeundwa na Nnauye kuchunguza sakata hilo la Mkuu wa Mkoa katika ripoti yake ilimkosoa Makonda na kuweka wazi alitumia vibaya mamlaka yake.

Hata hivyo kabla ya kutoka ripoti hiyo, Rais Magufuli alisema katika hotuba yake Jumatatu alipokuwa akizindua ujenzi wa barabara za ghorofa katika eneo la Ubungo Dar es Salaam kuwa Mkuu wa Mkoa aendelee kuchapa kazi na yeye hafanyi kazi kupitia maneno ya kwenye mitandao na kusisitiza kuwa yeye ndiye rais wa nchi.

XS
SM
MD
LG