Kuwait, ambayo imekuwa inajaribu kutafuta suluhu kwa njia ya amani ilikusaidia kushawishi mataifa ya ghuba ya uajemi kuondoa vikwazo dhidi ya Qatar, iliomba kuongezwa muda kuendelea kutafuta suluhu hadi Jumapili.
Kuwait iliomba muda zaidi, muda mfupi baada ya masharti yaliotolewa na muungano wa Saudi Arabia, ukiitaka Qatar iwe imewasilisha majibu, kukaribia kufikia kikomo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema leo na mashirika ya habari ya Kuwait na Saudi Arabia, imethibitisha kwamba muda umeongezwa mpaka mwisho wa Jumatatu.
Saudi Arabia, falme za kiarabu, Bahrain, na Misri zimetishia kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na kibiashara na Qatar toka Juni 5, zikishutumu serikali ya Doha kufadhili ugaidi na ushirika wake na Iran.