Chama hicho kilitarajiwa kupata viti 23 katika bunge hilo jipya, ambapo kimeshuka sana kutoka kwa idadi ya viti 53 kilivyokuwa navyo hapo awali. Gavana wa Tokyo Yuriko Koikie na chama chake cha Citizens First Party, pamoja na washirika wake, watashinda angalau viti 72 kwenye bunge hilo litakalokuwa na jumla ya viti 127.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kwamba uchaguzi huo wa Tokyo haukumhusu sana Koikie, bali ni kama kura ya maoni kuhusu Waziri mkuu Abe, ambaye anakabiliwa na tuhuma za kumsaidia rafiki yake kupata idhini ya kujenga taasisi ya masomo kuhusu tiba ya wanyama, katika eneo maalum la Kiuchumi, jambo amalo ni nadra kufanyawa katika serikali ya Japan.
Abe hata hivyo, amekanusha shutuma hizo, ambazo zimeshusha umaarufu wake.