Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 28, 2024 Local time: 08:43

Putin ziarani Vietnam akiendelea kutafuta uungwaji mkono


Rais wa Russia Vladimir Putin (Kushoto) akisalimiana kwa mkono na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha VietnamNguyen Phu Trong.
Rais wa Russia Vladimir Putin (Kushoto) akisalimiana kwa mkono na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha VietnamNguyen Phu Trong.

Russia na Vietnam ziliahidi Alhamisi kuimarisha uhusiano wakati Rais Vladimir Putin akifanya ziara ya kiserikali yenye lengo la kuiboresha mahusiano, ili kukabiliana na kutengwa kwa Moscow, na jumuiya ya kimataifa, kutokana na vita vya Ukraine.

Putin alisafiri hadi Vietnam, mshirika wa karibu wa Moscow tangu enzi za Vita Baridi, kutoka kwa mkutano mkuu na Kim Jong Un wa Korea Kaskazini, ambapo Kim aliahidi "uungaji mkono kamili" kwa Russia katika vita vyake dhidi ya Ukraine na wawili hao kutia saini mkataba wa ulinzi wa pande zote. Kiongozi wa Russia hakupata hakikisho la wazi kama hilo, la uungaji mkono kutoka Hanoi, lakini Rais wa Vietnam To Lam alionyesha ari ya kuimarisha ushirikiano wa kiulinzi.

"Pande zote mbili zinataka kuhimiza ushirikiano katika ulinzi na usalama, jinsi ya kukabiliana na changamoto za kiusalama kwa misingi ya sheria za kimataifa, kwa ajili ya amani na usalama duniani," Lam aliwaambia waandishi wa habari baada ya mazungumzo na Putin.

Forum

XS
SM
MD
LG