Putin amesema hayo wakati alipokuwa akifunguwa mkutano wa kwanza wa viongozi kati ya nchi yake na nchi za Afrika.
Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amsema kwamba Putin alipendekeza pia kuwa mpatanishi kati ya Ethopia na Misri kuhusu mzozo wa ujenzi wa bwawa kubwa barani Afrika katika mto Nile alipokutana na Rais Abdel Fatahh al Sisi na Waziri Mkuu wa Ethopia Abiy Ahed katika vikao mbali mbali.
Hata hivyo nchi hizo mbili zenye mvutano hazijaeleza msimamo wao kuhusu usuluhishi huo.
Mkutano huo uliofanyika katika mji wa mapumziko wa Sochi ulioko bahari ya Black Sea umehudhuriwa na viongozi kutoka nchi 54 za Afrika na zaidi ya wafanyabiashara 3000 wa Russia na Afrika.
Kando ya ukumbi wa mkutano kulikuwepo na maonyesho ya silaha na vyombo vya kijeshi vya Rashia yaliyokuwa na lengo la kushawishi nchi za Afrika kununua silaha za nchi hiyo.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.