Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 12:16

Polisi Nigeria wawaokoa watu wanne waliotekwa wengine 13 hawajapatikana


Polisi wakiwa katika kazi ya kuleta utulivu nchini Nigeria.
Polisi wakiwa katika kazi ya kuleta utulivu nchini Nigeria.

Polisi katika jimbo la Katsina, Kaskazini Magharibi  mwa Nigeria wamesema wamewaokoa  watu wanne ambao walitekwa na watu waliokuwa na silaha  kutoka kwenye msikiti  Jumamosi  jioni, na bado wanaendelea na kuwatafuta  watu wengine  zaidi ya 13.

Msemaji wa polisi katika jimbo la Katsina, Gambo Isah amesema Jumatatu, waumini bad hawajulikani walipo kutokana na shambulizi la kwenye msikiti ambapo wengi wao ni wanaume watu wazima.

Amesema wakati wa sala ya usiku ya Jumamosi watu wenye silaha wakiwa kwenye pikipiki aliuvamia msikiti wa Funtua ambao upo saa sita kaskazini mwa Abuja na kumpiga risasi Imam na mtu mwingine.

Akizungumza na Sauti ya Amerika kwa njia ya simu, Isah amesema, katika shambulizi hilo watu wawili wamejeruhiwa na wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali iliyoko katika jimbo hilo.

Siku hiyo ya tukio, wakati waumini walikuwa katika sala yao ya mwisho ya siku ile. Kabla ya kuwasili kwa kikosi chetu cha polisi, washukiwa wa shambulizi hilo walishatoweka wakiwa na baadhi ya waumini. Lakini juhudi za pamoja kati ya polisi na wanamgambo walifanikiwa kuwaokoa watu wanne. Kwa sasa hivi bado tunawatafuta waumini 13

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya jimbo hilo watu 40 hawajulikani walipo.

Shambulizi la msikitini ni tukio la karibuni la wimbi la utekaji nyara na kudai fidia katika eneo la Kaskazini mwa Nigeria, mamlaka inajitahidi kupambana na vitendo vya vurugu.

Mashambulizi yameongeza shinikizo kwa serikali ya rais Muhammadu Buhari kuimarisha ulinzi kabla ya uchaguzi mkuu wa Februari ambapo mrithi wa Buhari atachaguliwa .

Jeshi la polisi la Nigeria limeweka ulinzi mkali wakati wa kufunguliwa tena kwa njia ya reli ya Abuja-Kaduna.

Huduma za usafiri wa reli zilisimamishwa baada ya tukio la uvamizi la watu wenye silaha usiku wa tarehe 28 Machi ambapo abiria tisa waliuwawa na 62 kutekwa.

Wakati mashauriano yanaendelea ilishuhudiwa mateka wakiachiliwa pole pole kwa vikundi. Kundi la mwisho la mateka waliachiliwa mwezi wa Oktoba.

XS
SM
MD
LG