Mashitaka hayo yamekuja baada ya serekali kuwashutumu kuingine himaya ya bahari ya Nigeria bila kibali.
Shirika la habari la Reuters limeripoti kwamba nahodha wa meli anatokea India huku wafanyakazi wake wanatokea Poland, India, Sri-Lanka, na Pakistan kwa mujibu wa nyaraka za mahakama.
Baada ya kuombwa na serekali ya Nigeria, Equatorial Guinea, ilishikilia meli ya Heroic Idun, ambayo ina uwezo wa kubeba mapipa milioni 2 ya mafuta hapo Agosti 17 na kufanya safari bila kuwa na bendera ya utambulisho.
Meli hiyo ilikimbia kikosi cha bahari cha Nigeria, na kuingia katika himaya ya bahari ya Equatorial Guinea bila kuruhusiwa.
Watu hao 26 ikijumisha nahodha, walifikishwa katika mahakama ya mji mkuu wa jimbo la Rivers, Port Harcourt, Jumatatu na jana Jumanne.