Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:07

Papua New Guinea watumia miti na mikono kuwatafuta waathirika wa maporomoko ya Udongo


Watu wakiwa wamekusanyika baada ya maporomoko ya udongo katika kijiji cha Yambali . Picha na Emmanuel ERALIA / AFPTV / AFP.
Watu wakiwa wamekusanyika baada ya maporomoko ya udongo katika kijiji cha Yambali . Picha na Emmanuel ERALIA / AFPTV / AFP.

Wenyeji katika eneo la ndani kabisa huko Papua New Guinea walitumia fimbo na mikono yao kuchimba kwenye matope Jumatatu baada ya maporomoko makubwa ya ardhi ambapo inasadikiwa takriban watu 2,000 huenda wemefukiwa wakiwa hai, kanda za video zimeonyesha.

Mohamud Omer, mratibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji ameithibitisha Reuters kwamba kanda za video zilipigwa Jumatatu kwenye wadi ya Yambali katika jimbo la Enga.

Maporomoko makubwa ya ardhi yaliyotokea Papua New Guinea siku tatu zilizopita yamewazika zaidi ya watu 2,000, serikali imesema hivi leo, wakati njia mbaya na ugumu wa usafiri wa kupeleka misaada umepunguza matumaini ya kuwapata manusura.

Kituo cha Kitaifa cha Majanga kimetoa idadi mpya katika barua yake kwa Umoja wa Mataifa Jumatatu. Shirika tofauti la Umoja wa Mataifa limeweka uwezekano wa idadi ya vifo ni zaidi ya watu 670.

Tofauti hizo zinabainisha eneo la ndani la mbalo na ugumu wa kupata sahihi kuhusu makadirio ya watu. Hesabu rasmi ya watu katika taifa hiyo ilifanyika mwaka 2000 na wengi wanaishi katika vijiji vya milimani katika kisiwa hichoa cha Pacific.

Forum

XS
SM
MD
LG