Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 13:30

Pakistan yaahidi kutoelemea upande wowote katika mzozo wa Ukraine


Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistani Shah Mehmood Qureshi (Picha kwa Hisani ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistani)
Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistani Shah Mehmood Qureshi (Picha kwa Hisani ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistani)

Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Shah Mehmood Qureshi amepuuza maelezo kuwa msimamo wa nchi yake kutoelemea upande wowote katika mgogoro wa Russia na Ukraine unaharibu uhusiano wa Islamabad na Marekani au nchi za Magharibi, katika mahojiano na VOA Jumapili.

Nchi hiyo ya Kiislam ya Kusini mwa Asia yenye silaha za nyuklia imepinga shinikizo la Magharibi kuilaani Moscow kwa kuivamia Ukraine, badala yake inatetea kuwepo mazungumzo na diplomasia itumike kumaliza mgogoro huu.

Pakistan imedai kwamba inahitaji kukaa mbali na siasa za dunia ili iweze kuboresha mahusiano yake na nchi zote, ikiwemo Russia, na kukabiliana na changamoto zake za ndani.

“Hatutaki kuwa sehemu ya kundi lolote. Tumelipa gharama kwa kuwa katika makundi. Ndiyo maana tumekuwa waangalifu sana. Hatutaki kuchafua sifa yetu ya kutokuwa upande wowote, na ndiyo maana tumejizuia,” Qureshi aliiambia VOA.

“Njia pekee ya busara ni kutafuta suluhisho la kidiplomasia,” Qureshi alisisitiza, wakati akiongea kwa simu kutoka jimbo la Sindh lilioko kusini, ambako anahudhuria mkutano wa kisiasa wa chama chake tawala cha Pakistan Tehrik-e Insaaf.

Pakistan, mshirika mkuuwa Washington ambaye si mwanachama wa NATO, ilijizuilia wiki iliyopita kupiga kura kupitisha vyote azimio la Baraza la Usalama la UN la kuishutumu Russia kwa uchokozi wake dhidi ya jirani yake na piahaikupiga kura katika Mkutano wa Baraza Kuu ilolaani uvamizi huo. Pia nchi nyingine 34 nazo zilifanya hivyo hivyo, ikiwemo India, Sri Lanka na Bangladesh.

Balozi za Magharibi nchini Pakistan katika kilele cha Mkutano wa Baraza Kuu la UN kupiga kura wote kwa pamoja waliitaka nchi hiyo kulaani uvamizi wa Russia nchini Ukraine na kuunga mkono wito wa kimataifa kwa Moscow kusitisha vita mara moja.

Qureshi alisema madai ya kuwa nchi yake imeingia katika “kundi la Russia” ni za “uongo” na “ zimeeleweka kimakosa” maelezo ya kutokuwa upande wowote ya Islamabad kuhusiana na mgogoro wa Ukraine.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (Picha na Olivier Douliery/Pool via REUTERS)
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (Picha na Olivier Douliery/Pool via REUTERS)

“Nafikiri uhusiano wetu na Marekani ni mzuri. Tunaiona Marekani ni mshirika wetu muhimu na tungependa kuendelea kupata ushirikiano kutoka kwa Marekani,” alieleza.

“Pia nimeomba kuzungumza na [Marekani] Waziri [Mambo ya Nje Antony] Blinken na nimeambiwa kuwa yuko safarini kwa siku saba zijazo. Lakini nitakuwa na furaha zaidi kueleza mtazamo wa Pakistan [juu ya Ukraine] kwake,” Qureshi aliongeza.

Pia alipingana na ripoti kwamba mivutano ya kidiplomasia ya Pakistan na Washington imeongezeka kufuatia ziara ya mwezi uliopita ya Waziri Mkuu wa Pakistan, Imran Khan kuonana na Rais wa Russia Vladimir Putin.

Khan tayari alikuwa Moscow wakati Putin alipoamuru jeshi lake kuishambulia Ukraine. Lakini ziara hiyo iliripotiwa haikufurahiwa na Washington.

XS
SM
MD
LG