Harry alimfanyia Obama mahojiano mwezi Septemba 2017 ambayo ilitolewa kwenye matangazo ya Jumatano ya BBC.
Rais huyo mstaafu wa Marekani ambaye aliachia madaraka mezi Januari baada ya kuongoza kwa miaka minane, amesema kuwa ni muhimu wanaotumia mitandao watafute njia ya kuwasiliana ana kwa ana ili waweze kufahamiana
“Kwenye mitandao kila kitu kinapambwa, na unapokutana na watu ana kwa ana unagundua kuwa watu wanamatatizo yao,” Obama amesema.
Pia utagundua mambo yanayowauganisha watu kwa sababu unashuhudia kuwa mambo siyo mepesi hivyo kama yanavyoonyeshwa katika kumbi za mitandaoni.”
Amesema unapokutana na mtu ni vigumu kwako “ kuonyesha chuki na ukatili” kama vile inavyotokea kwenye mitandao.
Obama pia amesema kuwa kitu anachokikosa ni yale maisha ya kufanya kazi ya urais, “ kwa sababu ni kitu cha kupendeza,” lakini alikuwa anahisi “utulivu” baada ya kuacha madaraka na hivi sasa anaweza kujikita katika juhudi za kutafuta ufumbuzi wa masuala sugu kitu ambacho asingeweza kufanya alipokuwa ikulu ya White House kama rais.