Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 10:10

Niger yaondoa kinga ya kutoshitakiwa kwa Rais wa zamani


Rais wa zamani wa Niger, Mohamed Bazoum.
Rais wa zamani wa Niger, Mohamed Bazoum.

Mahakama ya juu ya Niger imeondoa kinga ya kutoshitakiwa rais aliyechaguliwa kidemokrasia Mohamed Bazoum, karibu mwaka mmoja tangu alipoondolewa madarakani na kundi la kijeshi waasi, wakili wake amesema Ijumaa.

Hatua hiyo sasa itafungua njia kwa utawala wa kijeshi kumshtaki kwa shutuma za uhaini. Bazoum na familia yake wamekuwa kwenye kizuizi cha nyumbani tangu mapinduzi ya kijeshi ysliyomuondoa madarakani mwaka jana. Kabla ya Bazoum kuondolewa madarakani kwa nguvu, Niger ilikuwa mshirika wa mwisho wa usalama na Magharibi katika Sahel, eneo kubwa la kusini mwa jangwa la Sahara, ambalo limekuwa ni kiini cha ghasia zenye msimamo mkali.

Lakini utawala wa kiesji uliamuru kuondolewa kwa majeshi ya magharibi kutoka nchini humo na kuligeukia kundi la mamluki la Wagner la Russia kwa msaada wa usalama. Wanajeshi wa Marekani wanatarajiwa kuondoka nchini humo ifikapo kati kati ya Septemba, Pentagon imesema mapema mwezi huu.

Wakili wa Bazoum, Reed Brody, amesema amekosoa uamuzi huo kuwa ni “dhihaka” kwa utawala wa sheria nchini Niger. Kundi la Human Rights Watch, limesema kuwa mawakili wa Bazoum wameshindwa kuwasiliana naye tangu Okotoba mwaka jana na kwamba wamenyimwamnafasi ya kuona stakabadhi za kesi yake.

Forum

XS
SM
MD
LG