Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 05:33

Nguli wa uchekeshaji Tanzania afariki


Marehemu King Majuto
Marehemu King Majuto

Mkongwe wa Tasnia ya filamu na uchekeshaji Tanzania, Amri Athumani maarufu kama King Majuto amefariki dunia katika hospitali ya Taifa Muhimbili Jumatano alipokuwa amelazwa katika kitengo cha mahututi (ICU).

Vyanzo vya habari nchini Tanzania vimesema Mzee Majuto alipelekwa nchini India kwa matibabu. Hata hivyo aliporejea Tanzania aliendelea na matibabu katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Mzee Majuto alizaliwa mwaka 1948 mkoani Tanga na kusoma shule ya Msambweni, mkoani humo. Marehemu Majuto alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 10.

Mzee Majuto ni muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda ya video na kuziuza kupitia Shirika la filamu Tanzania ( TFC).

Pia alikuwa mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho na vichekesho vyake aliyoshiriki katika nchi mbalimbali.

Pamoja na uchekeshaji King Majuto alikua mtunzi, mtayarishaji na mwandishi mzuri wa filamu. Kati ya filamu alizowahi kuigiza ni Mama Ntilie, Shoe Shine, Harusi ya Mboto, Mke wa mtu sumu, na Mfanya kazi Maskini.

XS
SM
MD
LG