Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 16:40

Nchi za Umoja wa Ulaya zimekubaliana kuongeza msaada wa kijeshi wa Ukraine


Mojawapo ya misaada ya kijeshi kwa Ukraine
Mojawapo ya misaada ya kijeshi kwa Ukraine

Mfuko huu ni tofauti na bajeti ya EU ambayo hairuhusiwi kufadhili shughuli za kijeshi. Uamuzi wa leo utahakikisha tena kwamba tuna fedha za kuendelea kutoa msaada wa kijeshi kwa vikosi vya washirika wetu, mwanadiplomasia wa juu wa kundi hilo, Josep Borrell aliongeza

Nchi za Umoja wa Ulaya zimekubaliana siku ya Jumatatu kuongeza msaada wao wa kijeshi kwa Ukraine kwa dola bilioni 3.8 hadi zaidi ya dola bilioni 13. Kituo cha Amani cha Ulaya-The European Peace Facility (EPF) ambacho nchi za EU zinachangia kulingana na ukubwa wa uchumi wao, tayari kimetenga dola bilioni 5 katika misaada ya kijeshi kwa Ukraine.

Mfuko huu ni tofauti na bajeti ya EU ambayo hairuhusiwi kufadhili shughuli za kijeshi. Uamuzi wa leo utahakikisha tena kwamba tuna fedha za kuendelea kutoa msaada wa kijeshi kwa vikosi vya washirika wetu, mwanadiplomasia wa juu wa kundi hilo, Josep Borrell, ambaye alikuwa ameomba fedha ziongezwe, alisema katika taarifa.

Kituo hiki kimethibitisha thamani yake. Imebadilisha kabisa jinsi tunavyounga mkono washirika wetu juu ya ulinzi. Hii inafanya EU na washirika wake, kuwa na nguvu, aliongeza kusema hivyo.

Waziri wa mambo ya nje wa Hungary, Peter Szijjarto alisema siku ya Jumatatu kuwa haitaondoa kizuizi cha dola milioni 546 za mfuko uliopo, hadi Kyiv itakapoondoa benki ya Hungary iliyoorodheshwa OTP kutoka kwenye orodha ya makampuni Kyiv ikiita wafadhili wa kimataifa wa vita vya Russia nchini Ukraine.

Forum

XS
SM
MD
LG