Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:18

Marekani yasema jaribio la mapinduzi Russia lafichia nyufa za utawala a Putin


Marekani Jumapili imesema uasi wa  muda mfupi wa kiongozi wa mamluki Yevgeny Prigozhin, dhidi ya uongozi wa kijeshi wa Russia, unaonyesha nyufa kubwa katika utawala wa miongo miwili wa rais Vladimir Putin na unahoji msingi wa vita vyake vya miezi 16 dhidi ya Ukraine.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, amekimbia kipindi cha “This Week” cha televisheni ya ABC, kwamba vita vimekuwa ni kushindwa kwa kimkakati kwa Putin katika karibu kila nyanja, kiuchumi, kijeshi, na msimamo wa kijiografia.”

Ameongeza kusema kwamba kumeonekana nyufa zikiibuka, hasa upinzani wa Prigozhin uanaomlenga Putin.

Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani amesema matokeo ya kundi la Wagner la Prigozhin, ya mapema Jumamosi huko Moscow kabla ya kurudi kwa ghafla karibu na mji mkuu wa Russia, bado ni picha ya kusisimua na matokeo yake ni ya uhakika.

Putin alimwita Prigozhin, mshirika wa muda mrefu ambaye wanajeshi wake walikuwa wakipigana pamoja na vikosi vya Russia, nchini Ukraine, msaliti kwa kugeuka dhidi ya utawala wake wa kimabavu.

Kisha kiongozi wa Russia, amesema Prigozhin hatashitakiwa na kumruhusu kwenda nchi jirani ya Belarus, mshirika wa Russia, chini ya mpango uliojadiliwa na kiongozi wa Belarus, Alexander Lukashenko. Lakini haikuwa wazi ikiwa Prigozhin, alikuwa amefika huko akiwa na kikosi cha mamluki pamoja naye.

Russia imesema mamluki wa Prigozhin ambao hawakujiunga na uasi wa muda mfupi wataruhusiwa kutia saini mikataba ya kupigana na jeshi la Russia, nchini Ukraine, lakini Blinken, amesema haijabainika nini kitatokea sasa kwa mamluki waliomfuata Prigozhin.

Forum

XS
SM
MD
LG