Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 16, 2025 Local time: 00:10

Nchi sita za Afrika kuanza kutengeneza chanjo za Covid kwa teknolojia ya mNRA - WHO


Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus.

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema leo Ijumaa kwamba nchi sita za Afrika zimechaguliwa kuanza utengenezaji wao wa chanjo za Covid-19 kwa kutumia teknolojia ya mfumo wa mRNA.

Kenya, Afrika Kusini, Nigeria, Senegal, Misri na Tunisia zilichaguliwa kuwa nchi za kwanza kupokea teknolojia ya mRNA kutoka kituo cha WHO cha kimataifa, katika bara ambalo, kwa kiasi kikubwa limeendelea kukabiliwa na changamoto za upatikanaji wa chanjo za ugonjwa huo.

Hatua hiyo, WHO inasema, ni katika msukumo wa kuhakikisha Afrika inaweza kujitengenezea chanjo zake za kupambana na Covid na magonjwa mengine.

Hafla ya Sherehe ya kutangaza uhamishaji wa teknolojia hiyo ya mRNA ilitarajiwa kufanyika Ijumaa mjini Brussels, Ubelgiji, katika mkutano wa mkuu kati ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika.

"Hakuna tukio lingine, kama janga la Covid-19 ambalo limeonyesha kuwa kutegemea makampuni machache kusambaza bidhaa za afya ya umma ulimwenguni ni hatari," mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema.

"Njia bora ya kushughulikia dharura za afya na kufikia huduma ya afya kwa wote ni kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa nchi mbalimbali, kutoa huduma za afya wanazohitaji," alisema.

Tedros ameendelea kutoa wito wa upatikanaji sawa wa chanjo ili kukabiliana na janga hilo, na kuyashutumu baadhi ya mataifa tajiri kwa kuhodhi dozi za chanjo, na kuifanya Afrika kusalia nyuma ya mabara mengine katika juhudi za kimataifa za kutafuta chanjo.

XS
SM
MD
LG