Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:01

Mvutano waongezeka Zimbabwe uchaguzi unavyo karibia


Nelson Chamisa, kiongozi wa muungano wa upinzani Zimbabwe (MDC), akiongea na waandishi wa habari Harare, Zimbabwe, Julai 12, 2018.
Nelson Chamisa, kiongozi wa muungano wa upinzani Zimbabwe (MDC), akiongea na waandishi wa habari Harare, Zimbabwe, Julai 12, 2018.

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imetahadharisha kuongezeka kwa mvutano wakati uchaguzi wa urais na bunge ukikaribia nchini Zimbabwe.

Ofisi hiyo pia imeiomba serikali na vyama vya kisiasa kuhakikisha kuwa uchaguzi unakuwa wa amani.

Julai 30 itakuwa ni uchaguzi wa kwanza Zimbabwe tangu rais wa zamani Robert Mugabe alipolazimishwa kuachia madaraka Novemba 2017 baada ya kutawala kwa miaka 37.

Ghasia ambazo zilikuwa zinaandaliwa na serikali ambazo kwa kawaida zilikuwa zikitokea wakati wa uchaguzi kwa miaka kadhaa ya utawala wa Mugabe hazijajitokeza wakati wa kampeni zinazoendelea kabla yauchaguzi

Msemaji wa ofisi ya Haki za Binadamu ya UN Liz Throssel amesema inatia moyo kuona kuwa mikutano ya kisiasa na maandamano ya amani yanafanyika katika mji mkuu, Harare, na pamoja na kuwepo matumaini jumuiya za kiraia zimetoa tahadhari.

“Bado tuna wasiwasi kwa kuongezeka ripoti, hasa katika baadhi ya maeneo ya vijijini, ya wapiga kura kutishiwa, vitisho vya uvunjifu wa amani, kubughudhiwa na ikiwemo kulazimishwa kuhudhuria mikutano ya kisiasa,” ameongeza.

Katiba ya Zimbabwe imetenga nafasi 60 za bunge kwa wanawake katika bunge lenye wajumbe 270. Pamoja na kuwepo mfumo huo wa idadi hiyo kisheria, Throssel amesema wanasiasa wagombea wanawake wanakabiliwa na upinzani na ukandamizaji na pia kukashifiwa.

“Hivi sasa matumizi ya lugha ya kashfa siyo kwamba itakuwa ni jambo la kushangaza,” amesema kuiambia VOA.

“Inawalenga wao kwa msingi wa kuwa ni wanawake, kwa kuwaita ni wanaharakati wa kike, ambao wanasema ni wagombea waliokuwa na viwango vya chini, na kuwashambulia wao binafsi.”

Mfumo wa Idadi maalum ulioko katika katiba, ambao utamalizika muda wake kabla ya uchaguzi wa 2023 tayari umesababisha wasiwasi juu ya mustakbali wa ushiriki wa wanawake katika siasa.

Maafisa wa Haki za Binadamu wa UN wamesema kuwa vurugu na aina nyingine za vitisho lazima visiruhusiwe kuharibu kile ambacho kinaweza kupelekea au lazima kitaleta mfumo wa haki wa uchaguzi ambao hauna vitisho kwa wananchi wa Zimbabwe.

XS
SM
MD
LG