Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:49

Jean-Pierre Bemba anatarajiwa kurudi DRC na kutangaza azma ya kugombea urais.


Makamu rais wa zamani wa DRC Jean-Pierre Bemba anatarajiwa kurejea nyumbani.
Makamu rais wa zamani wa DRC Jean-Pierre Bemba anatarajiwa kurejea nyumbani.

Kiongozi wa DRC na mbabe wa zamani wa kivita aliyefutiwa mashitaka ya uhalifu wa kivita mwezi Mei Jean-Pierre Bemba atarudi nchini mwake wiki ijayo kutangaza kugombea urais wa nchi hiyo afisa wa chama chake alieleza hayo jumatatu.

Kurudi kwake nyumbani baada ya kutumikia kifungo kwa miaka 10 huko The Hague kunaweza kubadili siasa za Congo kwa kiasi kikubwa kabla ya uchaguzi wa Desemba uliocheleweshwa ambao unatarajiwa kutafuta mrithi wa rais Joseph Kabila.

Kabila ambaye ameongoza tangu 2001 amekataa kueleza kama ataachia madaraka au la licha ya muda wake wa mihula miwili kumalizika mwaka 2016.

Washirika katika muungano wake hivi karibuni wameeleza madai yao kisheria ambayo yataruhusu ugombea wake.

XS
SM
MD
LG