Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:26

Museveni atangaza mkakati wa kufanya Kampala iwe mji wa kisasa, salama


Rais Yoweri Museveni
Rais Yoweri Museveni

Rais Yoweri Museveni amesema kuwa Kampala itaimarika kuwa salama katika miezi tisa ijayo wakati serikali ikichukuwa hatua ya kutekeleza vipengele vya suluhisho la kufanya uwe mji wa kisasa na salama kwa ajili ya nchi ya Uganda.

Hii ilikuwa ni sehemu ya hotuba ya Rais Museveni kwa taifa juu ya hali ya usalama akizungumza kutoka Entebbe, Jumamosi Jioni. Amesema kuwa Kampala itabadilika kuwa mji tofauti, ukiwa na usalama, usafi na wa kisasa.

Suluhisho hilo la kuufanya mji uwe salama na wakisasa litatekelezwa na jukwaa la mtandao unaounganisha vyombo vya usalama kuwa kitu kimoja likiwa na muonekano kamili, ambapo wadau wote, katika majukumu mbalimbali, idara au eneo wanalo fanya kazi watashirikiana kwa ajili ya kuboresha kukabiliana na uhalifu, pamoja na kuwepo uelewa zaidi wa mazingira na maboresho ya kusimamia matukio mbalimbali.

Rais Museveni anasema machine zina gharama ndogo kuliko binadamu na ameongeza kusema kuwa serikali itaendelea kuwategemea binadamu kwa kipindi kifupi na baadae itapunguza idadi ya binadamu wanaosimamia usalama.

Anasema mtu anapotembelea mji wa London, hivi sasa kuna matumizi zaidi ya teknolojia ukilinganisha na tegemezi la usalama unao simamiwa na binadamu.

Amesema amekasirishwa na mauaji ya Waganda wasio kuwa na hatia, na kuwa baada ya kupambana na wahalifu kwa vitendea kazi finyu, anasema utumiaji wa teknolojia iliyokuwa bora, utafanya uhalifu huu kuwa ni historia.

XS
SM
MD
LG