Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:47

Mshukiwa wa kuweka wazi nyaraka za siri za jeshi la Marekani akanusha mashtaka


Mchoro unaomuonyesha Jack Teixeira akiwa mahakamani.
Mchoro unaomuonyesha Jack Teixeira akiwa mahakamani.

Afisa wa kikosi cha kulinda mipaka ya bahari, wa jimbo la Massachusetts, Marekani, anayetuhumiwa kwa kuchapisha kinyume cha sheria, nyaraka za siri kali za kijeshi, kwenye mtandao wa kijamii, Jumatano alikanusha mashtaka ya uhalifu katika mahakama ya serikali kuu.

Jack Teixeira mwenye umri wa miaka 21, alisema hana hatia wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake, katika mahakama moja mjini Worcester, siku moja baada ya kufunguliwa mashitaka na jopo la mahakama, kwa makosa sita ya kuhifadhi kimakusudi, na kusambaza taarifa za ulinzi wa taifa.

Teixeira, mkazi wa mji wa North Dighton, amekuwa rumande tangu kukamatwa kwake mwezi Aprili mwaka huu, kwa tuhuma za utoaji wa siri za kijasusi, kesi ya kijasusi ambayo inaelezwa kuwa moja ya kubwa zaidi nchini Marekani.

Anatuhumiwa kuweka wazi nyaraka za kijeshi kuhusu vita vya Russia nchini Ukraine na masuala mengine nyeti ya usalama wa taifa kwenye mtandao wa kijamii wa Discord, unaopendwa sana na watu wanaocheza michezo ya mtandaoni.

Waendesha mashtaka wanasema aliendelea kufichua siri za serikali hata baada ya kuonywa na wakuu wake, kuhusu kushughulikia vibaya nyaraka za siri.

Wanasema kuwa hata baada ya kuonywa na wakuu wake mwaka jana, mshukiwa huyo alionekana tena mwezi Februari mwaka huu akitazama habari zisizohusiana na ujasusi, kinyume cha sheria.

Forum

XS
SM
MD
LG