Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:31

Mtu aliyevujisha nyaraka za siri za jeshi la Marekani akamatwa


Maafisa wa FBI wakimkamata Jack Taixeira, kuhusiana na uchunguzi wa uvujaji wa nyaraka muhimu za jeshi la Marekani, April 13, 2023.
Maafisa wa FBI wakimkamata Jack Taixeira, kuhusiana na uchunguzi wa uvujaji wa nyaraka muhimu za jeshi la Marekani, April 13, 2023.

Idara ya upelelezi ya Marekani (FBI) imemkamata mlinzi wa usalama wa anga mwenye umri wa miaka 21 kuhusiana na uvujaji wa mamia ya nyaraka muhimu za serikali ya Marekani na za kijeshi, mwanasheria mkuu Merrick Garland alitangaza Alhamisi.

Jack Teixeira, mfanyakazi kwenye kitengo cha ujasusi cha kikosi cha usalama wa anga katika jimbo la Massachusetts, alipelekwa kizuizini bila tatizo lolote kutoka makazi yake mjini North Dighton, jimboni Massachusetts, Alhamisi alasiri, FBI imesema katika taarifa.

Uchunguzi unaendelea, na FBI imesema maafisa wake waliendelea na shughuli za kisheria kwenye makazi yake.

Mwanasheria mkuu Garland alisema Teixeira alikamatwa kuhusiana na uchunguzi wa madai ya kuondoa bila idhini, kuhifadhi na kusambaza taarifa za siri za ulinzi wa taifa.

Chini ya sheria ya ujasusi, kuondoa bila idhini, kuhifadhi na kusambaza nyaraka muhimu ni kosa la jinai adhabu yake ni kifungo cha hadi miaka 10 jela.

XS
SM
MD
LG