Polisi wanamtafuta Frank R. James mtu mwenye ushawishi wakisema kuwa alikodi gari aina ya Van pengine inawezekana alihusika na shambulizi hilo.
Saa saba baada ya shambulizi la risasi gari hiyo iliondolewa kutoka eneo la tukio Jumanne usiku.
Wapelezi wamesisitiza kwamba hawakuwa na uhakika kama James alihusika na shambulizi la risasi.
James Essig, mkuu wa wapelelezi, anaeleza: "Mwanaume ambaye tunaamini kuwa alikodi gari hili la U- Haul huko Philadelphia ni Frank R. James, mwanaume mwenye umri wa miaka 62 akiwa na anwani ya Wisconsian na Philadelphia.
Tunamtufatua ili kujua kama anahusika na shambulizi kwenye treni. Matukio mawili ya uhalifu treni ya subway na van ni muhimu nab ado yanafuatiliwa.
Tunaomba kwa yoyote mwenye habari kusaidia kutoa taarifa , video zilizochukuliwa kwenye simu, taarifa za walioshuhudia, au vyovyote inavyoweza kutambua au mtu aliyekodi gari hili."
Maafisa wa usalama walikuwa wanaangalia machapisho ya James kwenye mitandao ya kijamii ambayo baadhi yalisababisha maafisa kuimarisha usalama kwa meya wa jiji la New York Eric Adams, ambaye kwa sasa amejitenga kutokana na maambukizo ya COVID -19.