Mpango huu ni matokeo ya mkutano wa New York wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa (UN) wa mwaka 2016.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wakuu wa mikoa ya Kigoma, Kagera, Tabora na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mataifa la Wakimbizi (UNHCR) pamoja na wadau wengine wanaowahudumia wakimbizi.
Katika uzinduzi huo uliofanyika Ijumaa, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni alisema utaratibu huu utawawezesha wakimbizi kuwa na fursa ya kupata huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
Aidha utakuwa na manufaa kwa Tanzania ambayo imekuwa ikibeba mzigo wa wakimbizi kwa miongo mitatu hadi hivi sasa.