Hatua hii ni sehemu ya mkakati wa kupambana na waasi wa kundi la M23 kwenye maeneo ya mashariki ya mlima wa Rutshuru, ambako kundi hilo limeweka kambi kwa karibu mwezi mmoja na nusu hivi sasa.
Wanajeshi hao kutoka Kenya na Tanzania wakiongozwa na kamanda kutoka India wamefuatana na wanajeshi wa Congo tangu jana hadi maeneo ya mapigano katika juhudi za awali za kuwataka wapiganaji wa M23 kuweka silaha zao chini, kabla ya kuamua kutumia nguvu.
Wakati huo huo kuna ripoti kwamba baadhi ya wapiganaji hao wameanza kujisalimisha na kukimbia kutoka k,undi hilo wakihofia maisha yao.