Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 06:33

Makundi ya waasi ya DRC hayana haraka ya kufanya mazungumzo na serikali


Wanajeshi wa serikali ya DRC wakipiga doria katika mapambano na waasi wa M23. PICHA: VOA/Austere Malivika
Wanajeshi wa serikali ya DRC wakipiga doria katika mapambano na waasi wa M23. PICHA: VOA/Austere Malivika

Baadhi ya makundi ya waasi yanayoshiriki mazungumzo ya kuleta amani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, yameomba mda zaidi kabla ya kuacha vita, ikiwa ni ishara kwamba mazungumzo hayo yanayoendelea Nairobi, Kenya, hayajapiga hatua muhimu.

Kulingana na taarifa ya ofisi ya rais wa Kenya, waakilishi wa makundi ya waasi 30 karibu 30, wanashiriki mazungumzo ya Nairobi, na wameomba mda zaidi kuthathmini kuhusu masharti ambayo yameekwa katika mazungumzo hayo, lakini wameeleza kwamba wapo tayari kushiriki katika ujenzi wa taifa hilo.

Makundi mengine wanayoshiriki mazungumzo hayo yamekubali juhudi za serikali ya Congo kushirikisha waliokuwa wapiganaji katika jeshi la nchi hiyo.

Hakuna taarifa zaidi zimetolewa kuhusu makundi ya waasi ambayo hayajakuwa tayari kushiriki vikamilifu katika mazungumzo hayo.

Wakati mazungumzo yalikuwa yanaendelea jiji Nairobi, Kenya, mapigano yamezuka tena mashariki mwa DRC karibu na mpaka na Uganda kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa M23.

Watu kadhaa wamekimbilia nchini Uganda.

XS
SM
MD
LG