Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 02:37

Mkutano wa nane kati ya China na wafanyabiashara wa Afrika wafanyika leo Beijing


Mkutano wa China na Afrika mjini Beijing, China.
Mkutano wa China na Afrika mjini Beijing, China.

Mkutano wa nane kati ya China na wafanyabiashara kutoka Afrika umeanza hii leo Ijumaa mjini Beijing, China, ikiwa ni sehemu ya mkutano mkuu unaonendelea kati ya viongozi wa Afrika na China.

Mkutano mkuu unaangazia ushirikiano wa kibishara kati ya China na Afrika.

Mkutano wa mwaka huu unaangazia namna ya kukuza viwanda na usambasaji wa bidhaa kwa kuzingatia ruwaza ya ushirikiano kati ya China na Afrika ya mwaka 2035 na ajenda ya maendeleo ya Afrika ya m waka 2063.

Kongamano limevutia zaidi ya washiriki 1000, wakiwemo wawakilishi 400 wa taasisi na biashara mbalimbali kutoka nchi 48 za Afrika zikiwemo Kenya, Senegal, na Afrika Kusini.

Kongamano hilo limefunguliwa wakati kikao cha viongozi wa Afrika kinakamilika leo Ijumaa.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewaambia viongozi wa Afrika kwamba ushirikiano mpana kati ya China na Afrika unaweza kupata suluhu ya nishati safi.

Katibu Mkuu akiwa katika Mkutano wa Ushirikiano wa China na Afrika, Beijing.
Katibu Mkuu akiwa katika Mkutano wa Ushirikiano wa China na Afrika, Beijing.

"Inaweza kuwa kichocheo cha mfumo muhimu wa chakula na digitali. Afrika ambao ni muhimu kwa uchumi wa nchi kadhaa duniani, inaweza kutumia fursa hiyo kupata msaada wa China katika kuimarisha biashara, usimamizi wa taarifa, fedha na teknolojia," alieleza zaidi Katibu Mkuu.

Forum

XS
SM
MD
LG