Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 19:31

Trump akaribia kufanya maamuzi ya mkataba wa Paris


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais wa Marekani, Donald Trump amesema atatangaza leo mchana uamuzi wake iwapo Marekani ijiondoe kwenye mkataba wa hali ya hewa wa Paris wa mwaka 2015.

Kwenye akaunti yake ya twitter jana usiku, Rais trump alisema atatangaza kwenye mkutano wake huko Rose Garden saa tisa mchana Alhamisi kwa saa za Washington DC.

Mwisho wa ujumbe wake alimalizia kwa msemo alioutumia kwenye kampeni yake wa “Make America Great Again”.

Mwanzoni mwa siku, kwenye picha akiwa na waziri mkuu wa Vietnam, Nguyen Xuan Phuc, Rais Trump alisema alikuwa akisikiliza maoni kutoka kwa watu wengi wa pande zote wakati anafikiria njia mbadala ya kufanya.

Msemaji wa Rais Trump, Sean Spicer amesema kwamba watu waliomshauri ni pamoja na viongozi wa biashara Marekani na wengine ni wakuu wa nchi za kigeni.

Mashirika mbali mbali ya habari yaliripoti jana Jumatano kwamba Rais ameamua kujiondoa kutoka mkataba wa ulimwengu, ambao umeidhinishwa na nchi 196.

Hatua kama hiyo itakuwa kubadilisha sera za enzi ya Obama, akiwaridhisha Warepublikan wenzake lakini ikiwakasirisha wanamazingira na washirika na wadau wengine wa mazingira nchini Marekani.

XS
SM
MD
LG