Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 22:23

Mike Johnson ndiye Spika Mpya wa Baraza la Wawakilishi la Marekani


Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani akizungumza baada ya kuchaguzliwa Oktoba 25, 2023.
Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani akizungumza baada ya kuchaguzliwa Oktoba 25, 2023.

Warepublican Jumatano walimchagua kwa shauku Mbunge Mike Johnson kama Spika mpya wa wa Baraza la wawakilish la Marekani, baada ya wiki kadhaa za malumbano yaliyosababisha shughuli mbalimbali kukwama baada ya kiti hicho kubaki wazi kufuatia kuondolewa kwa Spika wa zamani Kevin McCarthy.

Kiongozi huyo mhafidhina lakini asiyejulikana sana alipandishwa hadi kiti chenye hadhi kubwa katika uongozi wa Marekani, hatua ambayo kwa sasa inamaliza mgogoro wa kisiasa ya uliokuwa unakabili cahama chake.

Johnson, mwenye umri wa miaka 51, alipata kura 220 dhidi ya 209 alizopata mbunge Hakeen Jeffries wa chama cha Demokratik.

Akitokea jimbo la Louisiana, Johnson alishinda katika duru ya kwanza ya kura kwa uungwaji mkono kutoka kwa Warepublican wote waliokuwa na shauku ya kuweka nyuma ghasia za wiki zilizopita na kuendelea na uongozi.

Mwanachama wa ngazi ya chini wa timu ya uongozi wa baraza la wawakilishi ya chama cha Republikan, Johnson aliibuka mteule wa nne wa chama cha Republican katika kile ambacho kimekuwa mzunguko wa mzozo wa kisiasa tangu kuondolewa kwa Kevin McCarthy huku mirengo mbalimbali ya wanachama wa Republikan wakiwania mamlaka.

Johnson alikula kiapo baada ya kutoa hotuba fupi.

Ingawa hakuwa chaguo kuu la chama kwa nafasi ya Spika, Johnson, ambaye anaelezwa kuwa mwenye imani kubwa ya kidini ana mahasimu wachache na anaungwa mkono na rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump.

"Nadhani atakuwa Spika mzuri," Trump alisema Jumatano katika mahakama ya New York ambapo rais mwanasiasa huyo ambaye ni mgombea wa urais wa chama cha Republican mwaka wa 2024, anashtakiwa kwa madai ya udanganyifu wa kibiashara.

Mwanasiasa huyo anafahamika kwa shauku yake ya kuhamasisha Warepublikan kuuunga mkono juhudi za Rais wa zamani Donald Trump kubadilisha matokeo ya uchaguzi wa 2020.

Warepublikan walikuwa wamemteua Johnson baada ya mgombea mwingine, Mwakilishi Tom Emmer, kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho mapema Jumanne.

Johnson anakuwa spika wa 56 wa Baraza la wawakilishi katika historia ya Marekani.

Forum

XS
SM
MD
LG