Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 13:54

Mgombea wa urais nchini Venezuela akimbilia Uhispania kuomba hifadhi


Mgombea wa urais nchini Venezuela Edmundo Gonzalez
Mgombea wa urais nchini Venezuela Edmundo Gonzalez

Mgombea wa upinzani kwenye uchaguzi wa rais nchini Venezuela Edmundo Gonzalez alisafiri kuelekea Uhispania kuomba hifadhi, Madrid imesema.

Gonzalez aliikimbia nchi yake kutokana na mzozo wa kisiasa na kidiplomasia juu ya uchaguzi wenye utata wa mwezi Julai.

Gonzalez ambaye alipinga ushindi wa Rais Nicolas Maduro, aliwasili kwenye kambi ya kijeshi ya Torrejon de Ardoz pamoja na mke wake, wizara ya mambo ya nje ya Uhispania ilisema katika taarifa.

Kuondoka kwa mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 75 anayechukuliwa na Marekani, Umoja wa Ulaya na mataifa mengine ya eneo hilo kama mshindi wa uchaguzi, kunajiri wiki moja baada ya mamlaka za Venezuela kutoa hati ya kumkamata, zikimshutumu kupanga njama na uhalifu mwingine.

“Leo ni siku mbaya kwa demokrasia nchini Venezuela,” mkuu wa sera ya kigeni katika Umoja wa Ulaya Josep Borrell alisema katika taarifa.

“Katika demokrasia, hakuna kiongozi wa kisiasa anayepaswa kulazimishwa kutafuta hifadhi katika nchi nyingine.”

Makamu wa Rais wa Venezuela Delcy Rodriguez alisema kwenye Instagram kwamba mamlaka zilimpa njia salama Gonzalez kwa lengo la kurejesha “amani ya kisiasa.”

Forum

XS
SM
MD
LG