Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 29, 2024 Local time: 05:20

Mfame wa Jordan ateuwa kaimu waziri Mkuu baada ya kuvunjwa kwa serikali


Mfame Abdullah wa Jordan
Mfame Abdullah wa Jordan

Mfalme Abdullah wa Jordan amemteua msaidizi wa ngazi ya juu kwenye makao ya kifalme kuwa waziri mkuu baada ya serikali kujiuzulu mapema leo, mahakama ya kifalme imesema.

Hatua hiyo imechukuliwa ikiwa siku chache tu baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa bunge ambao upinzani wa kiislamu ulipiga hatua kubwa kwenye ufalme huo unaoungwa mkono na Marekani.

Hassan ambaye sasa ni mkuu wa ofisi ya mfame Abdullah, na ambaye alikuwa waziri wa mipango, sasa anachukua nafasi ya Bisher Khaswneh, mwanadiplomasia wa muda mrefu, na ambaye aliwahi kuwa mshauri wa kasri ya mfalme, aliyeteuliwa karibu miaka minne iliopita, taarifa zimeongeza.

Taarifa zimeongeza kusema kuwa Khaswneh atabaki kuwa kaimu hadi pale baraza jipya la mawaziro litakapoundwa. Hassan aliyesomea chuo kikuu cha Havard, na ambaye ni mtaalam anayeheshimika sana, ana kibarua kigumu cha kudhibiti athari za vita vya Gaza kwenye uchumi wa ufalme huo, ambao pia unashuhudia kushuka kwa idadi kubwa ya watalii wanaoutembelea.

Waziri mkuu aliyeondoka aliahidi kuleta mabadiliko yalioanzishwa na mfame Abdullah, ili kubadili ukuaji uliodumaa kwa takriban muongo mmoja.

Forum

XS
SM
MD
LG