Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 11:07

Meta: Mahakama Kenya yaamua kampuni mama ya Facebook inaweza kushtakiwa


META-FACEBOOK
META-FACEBOOK

Mahakama ya Kazi nchini  Kenya Jumatatu,  imeamuru kuwa Meta, kampuni mama ya Facebook, inaweza kushtakiwa katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki baada ya aliyekuwa  msimamizi  wa maudhui kufungua kesi dhidi ya kampuni hiyo akidai kufanya kazi katika mazingira magumu.

Kesi hiyo ambayo imefunguliwa na mtu mmoja kwa niaba ya kundi na pia inajumuisha madai dhidi ya kampuni ya nje ya Meta, Sama.

Kesi iliyofunguliwa inadai fidia ya fedha , na kuitaka kampuni iliyopewa usimamizi wa maudhui wawe na kiwango cha huduma ya afya na mishahara sawa na kile cha wafanyakazi wa Meta, kwamba haki za muungano wa wafanyakazi zilindwe na ofisi huria ya haki za binaadamu iwakague.

Maamuzi kutoka mahakama ya ajira na mahusiano ya kazi nchini Kenya, yanaweza kuathiri utendaji kazi wa Meta pamoja na wasimamizi wa maudhui duniani kote.

Nembo ya Jukwaa la Meta huko Davos, Switzerland, Mei 22, 2022.
Nembo ya Jukwaa la Meta huko Davos, Switzerland, Mei 22, 2022.

Kampuni hiyo ya Marekani inafanya kazi na maelfu ya wasimamizi wa maudhui duniani, waliopewa majukumu ya kukagua maudhui yaliyowekwa kwenye jukwaa lake.

Meta ilidai kuwa mahakama ya Kenya haikuwa na mamlaka ya kisheria kwa sababu kampuni haiko katika nchi hiyo ya Afrika, na hivyo itolewe katika kesi hiyo.

"Kwa kuwa ombi hilo limeibua masuala fulani ambayo bado hayajaamuliwa, haitafaa kwa nchi kuwafutilia mbali wahojiwa hao wawili kwenye madai hayo” Jaji Jacob Gakeri alisema katika uamuzi wake siku ya Jumatatu.

Meta haijatoa majibu ya mara moja kuhusu suala hilo. Aliyekuwa msimamizi wa maudhui Daniel Motaung, ambaye alifungua kesi hiyo, amasema mazingira ya kazi yamemsabishia ugonjwa wa msongo wa mawazo (PTSD).

Awali, Meta ilishakabiliwa na kesi za usimamizi wa maudhui. Suluhu kati ya Facebook na zaidi ya maudhui 10,000 ambao walidai kuwa kampuni hiyo imeshindwa kuwalinda dhidi ya majeraha ya kisaikilojia ambayo yamesababishwa na wasimamizi ambao waliishutumu kampuni kwa kushindwa kulinda dhidi ya majeraha ya kisaikolojia yaliyotokana kuona picha za ngono na za ukatili.

Meta pia inakabiliwa na kesi nyingine nchini Kenya. Mnamo Desemba, watafiti wawili wa Ethiopia na kundi la haki za Kenya waliwasilisha kesi wakiishutumu Meta kwa kuruhusu machapisho ya vurugu na chuki kutoka Ethiopia ambayo yalishamiri kwenye Facebook, na kuchochea vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Ethiopia.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la Habari la Reuters.

XS
SM
MD
LG