Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 07:28

Membe ajiunga rasmi na ACT Wazalendo


Bernard Membe
Bernard Membe

Mwanasiasa Mkongwe nchini Tanzania Bernard Membe ametangaza Jumatatu kujiunga na chama cha ACT Wazalendo.

Katika mazungumzo na vyombo vya habari kwa njia ya mtandao Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe alimtambulisha mwanasiasa huyo kama mwanachama wao mpya.

Katika mazungumzo yake na vyombo hivyo Bernard Membe mwenyewe alishiriki na kueleza kuwa tarehe 6 Julai alikwenda katika ofisi za tawi la ACT wazalendo RONDO na kujisajili.

Zitto amesema : "Ningependa kumtambulisha rasmi Bernard Membe kawa mwanachama wetu mpya ambaye aliwahi kuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania. Wiki iliyopita alitembelea tawi letu Kijijini kwao Rondo kusini mwa Tanzania na kujisajili kuwa mwanachama wetu. Kutokana na utamaduni wake, jithada zake lakini kutokana na utashi wake katika masuala ya Haki za binadamu, kusimamia ukweli, uongozi na siasa tunaona ni hatua kubwa na nikaona niwajulishe hili."

Akizungumza katika mkutano huo Membe ameeleza azma yake ya kushiriki kutaka kuwa na mchango wa kuleta mabadiliko kwani Tanzania inayahitaji na kwamba atashiriki katika uchaguzi mkuu mwaka 2020.

Bernard Membe alisema : "Ni heshma kubwa kwangu kuwa mwanachama wa ACT Wazalendo,natarajia kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao, taifa letu linahitaji mabadiliko sasa, nitatumia uzoefu wangu wa miaka tisa na nusu kama Waziri wa Mambo ya nje kukisaidia chama changu kutengeneza sera zitakazoisaidia Tanzania kutokua taifa linalotazamwa kwa ubaya na jumuiya za kimataifa, na kuirejeshea heshma yake kama awali. Kuwarudisha wawekezaji na kuboresha uchumi ili kuiweka Tanzania kuwa kiongozi katika uimarishaji utangamano katika nchi za Maziwa Makuu."

Kwa mujibu wa Zitto Kabwe Bernard Membe atatambulishwa kesho kwa wanachama na Watanzania .

XS
SM
MD
LG