Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:26

Meli imeshaanza safari Kenya isonge mbele - Balozi wa Marekani


Balozi Robert Godec
Balozi Robert Godec

Balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec Jumamosi alionyesha kuunga mkono ajenda ya maendeleo ya Rais Uhuru Kenyatta na kutoa wito kwa vyama vya upinzani kumuunga mkono rais.

Godec amesema mjadala wa kitaifa lazima uhamie katika kuangalia changamoto zinazoikabili Kenya na siyo siasa za uchaguzi za mwaka 2017.

“uchaguzi umemalizika na ni wakati sasa wa nchi kupiga hatua kwa kukuza uchumi na maendeleo,” amesema wakati alipomtembelea Spika wa Baraza la Seneti la Kenya, Kenneth Lusaka katika Majengo ya Bunge.

Amesema kuwa Marekani itaendelea kuunga mkono na kushiriki katika programu ya Rais Uhuru ya nguzo nne za maendeleo.

Godec amezungumza wakati ambapo Umoja wa Upinzani NASA ukiwa katika uzinduzi wa kumuapisha Raila Odinga ifikapo mwisho wa mwezi wa Januari.

NASA imekuwa ikishinikiza kuwepo kwa mazungumzo ya haki ya uchaguzi kwa madai ya kuwa uchaguzi wa urais wa mwaka Agosti 2017 na Octoba 26 ulikuwa siyo halali.

XS
SM
MD
LG