Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 19:36

McMaster asema 'hatikiswi' na repoti za mawasiliano ya Kushner


McMaster na Jared Kushner
McMaster na Jared Kushner

Mshauri wa Usalama wa Taifa HR McMaster amesema Jumamosi kuwa kile kinachosemwa ni “mawasiliano yasio rasmi” ni kitu cha kawaida.

Alikuwa akiulizwa kuhusu repoti ya gazeti la Washington Post inayosema kuwa mkwe wa Rais Donald Trump alikuwa amejaribu kutengeneza njia za mawasiliano ya siri na Russia kabla ya rais kuingia madarakani..

McMaster ambaye alikuwa Taormina, Italy kwenye mazungumzo yanayofanyika pembeni ya mkutano wa G7, hakutaja lolote kuhusu Jared Kushner, ambaye pia ni mshauri wa ngazi ya juu wa Trump.

Alipoulizwa iwapo atapata wasiwasi, kukiwa na taarifa kwamba katika uongozi huo kuna mtu alikuwa anajaribu kufanya mawasiliano ambayo siyo rasmi na ubalozi wa Russia au Kremlin, McMaster alijibu “hapana.”

“Tuna mawasiliano ambayo siyo rasmi na baadhi ya nchi. Kwa ujumla kuhusu mawasiliano yasiyo rasmi inachokuwezesha ni kuwasiliana kwa njia ya usalama,” amesema McMaster.

Gazeti hilo limemnukuu afisa wa Marekani Ijumaa akisema kuwa kitendo hicho cha kuomba mawasiliano ya faragha kilikusudia kulinda mazungumzo yao kabla ya kuapishwa rais ili yasichungunzwe.

Vyanzo vya habari vya gazeti hilo vimesema balozi Sergei Kislyak ameripoti kwa wakubwa zake Moscow kuwa Kushner alitoa pendekezo hilo wakati wa mkutano wao mapema Disemba wakiwa katika Jumba la Ghorofa la Trump huko New York City.

Vyanzo hivyo vimesema taarifa hiyo ilinaswa kupitia mazungumzo ya Russia ambayo yalipitiwa na maafisa wa Marekani.

Siku ya Alhamisi, vyombo vya habari viliripoti kuwa Kushner anachunguzwa na FBI katika utafiti wao kuwa inawezekana kuwa kulikuwa na ushirikiano (wa udukuzi) kati ya kampeni ya Trump na Russia.

Gazeti hilo limeripoti pia wiki iliyopita kwamba afisa wa ngazi ya juu wa White House ambaye yuko karibu na rais alikuwa ndiye mlengwa muhimu katika uchunguzi huu uliokuwa nyeti, japokuwa haukutaja kwamba mtu huyo ni Kushner katika kipindi hicho.

Uchunguzi wa FBI hivi sasa unavyomfuatilia Kushner haimanishi kwamba lazima ni mshukiwa wa jinai, na wala hachukuliwi kuwa ndiye mlengwa wa uchunguzi mpana zaidi wa FBI dhidi ya Russia.

XS
SM
MD
LG