Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:49

Mbunge wa NRM auwawa Uganda


Gari ya Ibrahim Abiriga iliyoshambuliwa kwa risasi nchini Uganda
Gari ya Ibrahim Abiriga iliyoshambuliwa kwa risasi nchini Uganda

Mbunge wa manispaa ya Arua, Ibrahim Abiriga ameuawa kwa kupigwa risasi kadhaa na watu wasiojulikana, karibu na nyumbani kwake, Kirinyabigo mtaa wa Kawanda,wilayani Wakiso, karibu na jiji la Kampala.

Mlinzi wake aliyekuwa amevalia sare za kijeshi naye amauawa baada ya gari lao kumiminiwa risasi kadhaa.

Kulingana na walioshuhudia tukio hilo,watu waliokuwa wamefunika nyuso zao, wakitumia usafiri wa pikipiki, wamemimina risasi kwenye gari la Abiriga kabla ya kutoroka.

Mara kadhaa, Abiriga amekuwa akisema kwamba usalama wake umekuwa hatarini. Amekuwa akisema kwamba watu wengi hawana furaha kwamba anamuunga mkonorais Museveni, hasa baada ya mabadiliko ya katiba.

Matamshi yake hata hivyo yamekuwa yakichukuliwa kama mzaha, kwani usemi wake umekuwa na ucheshi mwingi kila mara.

Wakati mmoja, aliwaeleza waandishi wa habari kwamba alikuwa ameamua kujinunulia pistol, kwa sababu anahofia maisha yake

Abiriga amekuwa mmoja wa wabunge wazalendo kwa rais Yoweri Museveni, kiasi cha kuvalia nguo za rangi ya manjano, kuendesha gari la rangi ya manjano na kila kitu chake ni cha rangi ya manjano, ambayo ni rangi ya chama tawala cha NRM, cha raisMuseveni.

Alikuwa miongoni mwa wabunge walioshinikiza mabadiliko ya katiba yaliyotoa fursa kwa rais Yoweri Museveni kuwania tena urais,kwa kuondoa kizuizi cha umri.

Abiriga ambaye alikuwa na umri wa miaka 62 amekuwa mbunge wa chama tawala cha NRM, alikuwa Kapteni katika jeshikabla ya kuingia katika siasa.

Waziri wa habari na mawasiliano Frank Tumwebaze, kupitia kwa mtandao wake wa Twitter, amekitaja kifo cha Abiriga kuwa cha kuumiza moyo huku msemaji wa rais Yoweri Museveni,Don Wanyama akisema kwamba wale ambao wamemuua Abiriga kwa kumwaga damu, nao damu yao itamwagika.

XS
SM
MD
LG