Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 20:58

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa China na Australia wakutana mjini Canberra


Waziri wa mambo ya nje wa China, Wang Yi akiwa na mwenzake wa Australia ,Penny Wong, mjini Canberra, Australia. Machi 20, 2024.
Waziri wa mambo ya nje wa China, Wang Yi akiwa na mwenzake wa Australia ,Penny Wong, mjini Canberra, Australia. Machi 20, 2024.

Waziri wa mambo ya nje  wa China Wang Yi, Jumatano amekutana na mwenzake wa Australia Penny Wong mjini Canberra, ikiwa ni  dalili ya kuimarika kwa  uhusiano ya mataifa hayo jirani, kwenye eneo la Asia Pacific.

Ziara ya Wang nchini Australia ni ya kwanza ya afisa wa ngazi ya juu wa China tangu 2017. Uhusiano kati ya Beijing na Canberra kwa mara ya kwanza ulionekana kudorora pale Australia ilipopiga marufuku mpango wa kampuni kubwa ya mawasiliano ya China ya Huawei, kutengeneza mtandao wa 5G nchini humo.

Hali iliendelea kuwa mbaya baada ya Australia kushinikiza uchunguzi huru kuhusu chanzo cha janga la COVID-19, ambapo kwa mara ya kwanza ugonjwa huo uligunduliwa katikati mwa China mwaka 2019. China kwa upande wake ilijibu kwa kuweka ushuru mkubwa na masharti kwa bidhaa za Australia kama vile shayiri, nyama, makaa ya mawe, na mvinyo, hatua ilioathiri pakubwa uchumi wa Australia.

Wakati wakiongea na wana habari baada ya kikao chao, Wong amesema kwamba yeye na Wang wamejadili kuhusu hali ya mwandishi wa Australia mwenye asili ya China, Yang Hengjun, ambaye ameendelea kushikiliwa Beijing tangu 2019, kwa tuhuma za ujasusi.

Mahakama ya China ilimhukumu adhabu ya kifo iliyositishwa dhidi ya Yang hapo Februari. Wong amesema kwamba amemwambia mwenzake wa China kwamba watu wa Australia walishtushwa sana na hukumu hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG