Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:11

Mauaji ya Waislam Myanmar yawekwa wazi na ripoti ya UN


Mwanamke mkongwe wa jamii ya Waislam wa Rohingya ambaye ni mkimbizi akiwa taabani baada ya kuvuka mpaka kuingia Bangladesh
Mwanamke mkongwe wa jamii ya Waislam wa Rohingya ambaye ni mkimbizi akiwa taabani baada ya kuvuka mpaka kuingia Bangladesh

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi anakabiliwa na swala zito la Waislam wa Rohingya ambao wamekimbilia India baada ya kutokea mauaji ya kinyama dhidi yao nchini Myanmar.

Vyanzo vya habari nchini Myanmar vinaeleza kuwa Waislam wa nchi hiyo wamekuwa wakikimbia kuelekea India na Bangladesh.

Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, helikopta za kijeshi zimeendelea kupiga risasi maeneo ya Waislam.

Ripoti hiyo pia inasema kuwa kwa miaka 10 iliyopita, Jeshi la nchi hiyo limekuwa likiwatafuta watu wazima wa jamii hiyo ya Waislam na kuwaua na ndiyo sababu watu wa Rohingya wanakimbilia Bangladesh. Hata hivyo serikali ya Myanmar imekanusha tuhuma hizo dhidi ya Jeshi lake.

Kwa mujibu wa ripoti ya taasisi zinazoshughulikia wakimbizi zikifanya kazi na Umoja wa Mataifa, kiasi cha Waislam wa Rohingya 400 waliuawa wakati wa machafuko hayo na wakati upelelezi ukifanywa na Jeshi.

Kufuatia mauaji hayo Takriban Waislam 40,000 wameondoka kutoka katika makazi yao huko Myanmar na sasa wanapata hifadhi katika majimbo ya Hyderabad, Jammu, Delhi, West Bengal, Uttar Pradesh, Punjab na Rajasthan nchini India.

Masiku machache yaliyopita, Waziri wa Nchi wa India (Mambo ya Ndani ) Kiren Rijiju alisema kuwa Waislam wote wa Rohingya wanaoishi India wataondolewa kurejeshwa makwao. Tangazo hili la serikali linatathminiwa kufuatia ziara ya Waziri Mkuu wa India nchini Myanmar.

Viongozi wa Waislam wa Rohingya wameiomba Mahakama ya Juu kutowarejesha Waislam waliokimbilia India kutokana na sababu ya haki za kibinadamu. Hivi sasa, Mahakama ya Juu imeiambia serikali kuweka wazi msimamo wake juu ya swala hilo.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari ulimwenguni, mauaji haya dhidi ya Waislam wa Rohingya sio kitu kipya huko Myanmar—ambapo siku za nyuma ilikuwa inajulikana kama Burma.

Lakini tukio hili la karibuni limekuza mgogoro huo nakuleta wasiwasi mkubwa juu ya usalama wa Waislam hao.

Mnamo Agosti 25, wapiganaji wachache wa Rohingya walishambulia dazeni ya vituo vya polisi na kambi za kijeshi nchini Myanmar. Kikundi cha wapiganaji kinachojiita Arakan Rohingya Salvation Army kilidai kuhusika na mashambulizi hayo.

Kufuatia upelelezi uliofanyika, Jeshi la nchi hiyo liliunguza nyumba 2,600 za Waislam wa Rohingya jambo ambalo limefanya zaidi ya Waislam 125,000 kukimbilia Bangladesh kuokoa maisha yao.

Inaelezwa kuwa Waislam wa Rohingya wanakandamizwa kuliko jamii yoyote duniani.

Myanmar ni taifa la watu walio wengi wenye kufuata madhehebu ya Buda

Takriban Waislam wa Rohingya milioni 1 wanaishi katika jimbo la Rakhine huko Myanmar.

Waislam hawa wanasadikiwa kuwa ni wakimbizi kutoka Bangladesh na ndio sababu serikali ya Myanmar haiwatambui kama raia wa nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG