Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 22:07

Amnesty International yafichua mauaji ya SPLA Sudan Kusini


Rais Salva Kiir
Rais Salva Kiir

Repoti mpya ya Shirika la haki za binadamu (Amnesty International) inasema kuwa askari wa Jeshi la Sudan Kusini (SPLA) wamefanya mauaji dhidi ya raia wake.

Ripoti hiyo pia imeeleza kuwa majeshi hayo yamechoma moto majumba, yameua raia na kuiba mali zao katika mkoa wa Upper Nile kati ya Januari na Mei wakati walipokuwa wanapambana na vikundi vya waasi..

Taasisi ya Uingereza inayoshughulikia haki za binadamu imesema iliwasaili watu 79 walioathiriwa na unyama huo, na mashuhuda ambao wamesema vikosi vya serikali na wanamgambo wake waliwalenga raia na kuwaibia majumbani mwao, kufuatia janga la mashambulizi hayo.

Shirika la Amnesty International limesema zilikusanya picha za satellite zilizoonyesha uharibifu huo wa majumba ya raia na mali zao katika eneo la kati la Wau-Shilluk.

Kikundi hicho kimeomba msaada wa kibinadamu wa dharura ufikishwe kwa wananchi hao na pia watu walioondolewa katika maeneo yao kutokana na vita hiyo wapatiwe hifadhi.

Naibu msemaji wa SPLA, Kanali Santo Domic Chol ameikataa ripoti hiyo na kusema inaikandamiza serikali.

Amesema vikosi vya serikali haviwezi kulenga au kufanya mauaji dhidi ya raia.

“Hii ripoti ni kandamizi. Hii ni propaganda kamili. Watu wanazungumza kutoka New York; watu wanazungumza kutoka wapi, huu ni upuuzi mtupu,” Chol amesema.

Kuanzia Januari mpaka Mei 2017, serikali imeendesha mashambulizi katika eneo la Upper Nile na kuichukua ardhi ilikuwa chini ya himaya ya kikundi chenye silaha cha wapinzani kinachojumuisha wapiganaji wa Agwelek chini ya usimamizi wa Jenerali Johnson Olony.

Uvunjifu wa amani ulipelekea maelefu ya raia kulazimika kuhama katika maeneo yao, na hivyo kuanzishwa kambi ya muda kwa ajili ya wanaokimbia maeneo yao huko Aburoc.

XS
SM
MD
LG