Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:43

Mateka 43 wa ADF warejeshwa katika maisha ya kawaida mashariki mwa DRC


Watu walionusurika katika shambulizi baya la ADF katika mji wa Beni, Novemba 29, 2019. Picha ya AFP
Watu walionusurika katika shambulizi baya la ADF katika mji wa Beni, Novemba 29, 2019. Picha ya AFP

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatano liliiambia AFP kwamba mateka wa zamani 43 wa kundi la ADF lenye uhusiano la Islamic State waliookolewa na majeshi ya Congo na Uganda wamerejea katika maisha ya kawaida.

Jeshi la Congo Jumanne liliandaa hafla katika mji wa mashariki wa Beni kwa ajili ya raia hao 43, wakiwemo wanawake 16 na watoto 24.

Waliachiliwa miezi sita iliyopita katika operesheni ya pamoja kati ya Jeshi la Uganda na la Congo, baada ya kutekwa nyara na waasi wa ADF, msemaji wa jeshi la congo katika jimbo la Kivu Kaskazini, Luteni Kanali Mak Hazukay alisema.

Shirika la kiraia litawasaidia watu wazima, nao ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC unawasaidia watoto kuzowea kuishi katika maisha ya kiraia.

ADF, ambayo ilikuwa inaundwa awali na waasi wa Uganda wengiwao wakiwa waislamu, iliimarisha kuwepo kwake mashariki mwa Congo katika miongo mitatu iliyopita, na kuua maelfu ya raia.

Forum

XS
SM
MD
LG