Idadi hiyo imeshuka kwa asilimia 9 ikilinganishwa na watu 130 waliouawa mwaka 2022, huku idadi ya watu waliotoweka ikipungua kwa zaidi ya asilimia 50 katika kipindi hicho, ripoti hiyo imesema.
Nusu ya mauaji hayo yalifanyika wakati wa operesheni za kupambana na uhalifu, kulingana na ripoti ya mashirika ambayo ni pamoja na Human Rights Watch, Amnesty International Kenya na kundi la Kenya la Missing Voices.
Watu wengine 45 waliuawa wakati wa maandamano yaliyoitishwa na upinzani nchini Kenya kati ya mwezi Machi na Julai mwaka jana kupinga gharama ya juu ya maisha, mashirika hayo yamesema.
Msemaji wa polisi Resila Onyango hakujibu ombi la shirika la habari la AFP la kutoa maelezo kuhusu ripoti hiyo.
Forum